Amehitimu elimu ya chuo kikuu, na amehudumu kwa takribani miaka 25 ya kazi kusaidia wengine wafanikiwe akiwa katika nafasi ya mkuu wa idara. Katika kipindi hiki amehudumu kwenye makampuni matatu ya kimataifa. Hivyo anao uzoefu katika sekta ya kilimo biashara na usindikaji kwa miaka 7, wa kuzalisha vyakula na usambazaji kwa miaka 8, na uagizaji na uuzaji wa mafuta kwa takribani miaka 10. Kwa sasa ni mhudumu katika biashara ya kilimo cha matunda, na usambazaji huu wa vitabu.
Kitabu Uumbaji wa Mtu; kinaanzia na YAHWEH Katika Milele kuchambua yapi na vipi vilipelekea kuumbwa kwa ulimwengu, na hatimaye pawepo mahali wakati ambapo mtu angeweza umbwa na kuishi humo. Ndipo tunaonyeshwa Kuumbwa kwa Roho na Nafsi ya Mtu katika milele, kabla kabisa ya Kufanywa kwa Mwili Mme na Mke, kwa minajili ya mtu katika hali ya roho-nafsi ahifadhiwe humo.
Mpango wa Ukombozi unaonyeshwa kama matokeo ya kuhakikisha uhitaji wa Mungu YAHWEH kuwa na familia unakamilika. Na hili lilijulikana na kupangwa kabla ya uanguko wa mtu duniani. Hivyo tokea ufahamu huu, tunachungua kwa kina Tafsiri na Asili ya Uasi na Dhambi, na hususani Kudanganywa kwa Havaa (Eva) na Uafiki wa Adam. Kuhitimisha haya yote tunafanyia uhakiki Dhana ya Dhambi ya Asili. Pamoja na haya ni mengi mengine ya kushangaza na kustaajabisha kuhusu Uumbaji wa Mtu.
Katika haya tunajibu sababu ya uwepo wako hapa duniani, na maalumu kabisa ni yapi ndiyo wajibu na majukumu yako kama mtu. Na bila kupoteza muda tunafanyia mapitio nadharia kadhaa za uumbaji, kuthibitisha kweli ya maandiko matakatifu. Kitabu chafaa sana kwa Mafundisho ya kitaaluma.
Título : Uumbaji wa Mtu
EAN : 9798227559371
Editorial : Shannel Steven Silwimba
El libro electrónico Uumbaji wa Mtu está en formato ePub protegido por CARE
¿Quieres leer en un eReader de otra marca? Sigue nuestra guía.
Puede que no esté disponible para la venta en tu país, sino sólo para la venta desde una cuenta en Francia.
Si la redirección no se produce automáticamente, haz clic en este enlace.
Conectarme
Mi cuenta