Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.
Elimu ya juu aliipata chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.
Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni.
Furaha ya kupiga hatua kubwa kwenye maendelezo, hasa usafirishaji wa ardhini kwa njia ya kisasa. Ilitumbukia nyongo baada ya safari ya uzinduzi wa treni ya umeme ya kisasa kuanza. Ikiwa ni siku muhimu sana kwa nchi nzima.
Habari ikafikishwa treni nzima ilitegwa bomu la kisasa, lililounganishwa kwenye mfumo wa umeme wa chombo hicho. Ikitokea kama ikasimamishwa, kupunguza mwendo au kuongeza zaidi ya uliyopo. Basi hakuna ambaye angesalia mule ndani.
Rais wa nchi nzima alipewa masharti kadhaa ikiwemo kumwachia huru mhalifu hatari sana, ambaye kashikiliwa na majasusi wa EASA na kufungwa au kutolewa kwake wao ndiyo wenye amri pekee. Sheria ya kuundwa kwa shirika lile la majasusi, iliweka wazi hakuna Rais wa nchi mwanachama wa Afrika ya mashariki aliye na mamlaka ya kuingilia operesheni zake
Título : Septemba Mosi
EAN : 9798227017758
Editorial : Mambosasa
El libro electrónico Septemba Mosi está en formato ePub
¿Quieres leer en un eReader de otra marca? Sigue nuestra guía.
Puede que no esté disponible para la venta en tu país, sino sólo para la venta desde una cuenta en Francia.
Si la redirección no se produce automáticamente, haz clic en este enlace.
Conectarme
Mi cuenta