Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.
Elimu ya juu aliipata chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.
Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni.
Balaa linaanza baada ya Norbert Kaila kupokea wito wa kushiriki uandishi wa kitabu. Akikubali wito huo aliyempatia alimwazima gari yake kwenda kuchukulia mzigo. Mwishowe inakuja kukutwa ilihusika kusafirisha mzigo wa madawa ya kulevya kutoka ufukweni hadi kwenye nyumba fulani.
Hajakaa sawa alipokea taarifa ya kusakwa na polisi kila kona, huku yule aliyempa gari akijulishwa amefariki kwa ajali ya gari. Mambo yalizunguka vibaya mno, inambidi aingie kazini kujisafisha na pia amshawishi Inspekta Ali Bongo aliyekuwa akishughulika na kesi ya waliyoshikwa na madawa ya kulevya. Ahakikishe anaamini hana hatia kwenye suala hilo, jambo ambalo linamfanya atumie ujuzi wake.
Kimbembe yule bwana ambaye alitaka kufanya kazi naye, alimwachia muswada wa kitabu husika ambao ulibeba mazito mno na alikuja kubaini ndiyo chanzo kikuu cha kifo chake. Naye anawaletea Kisanga kizito wauza unga
Título : Kisanga
EAN : 9798227981653
Editorial : Mambosasa
El libro electrónico Kisanga está en formato ePub
¿Quieres leer en un eReader de otra marca? Sigue nuestra guía.
Puede que no esté disponible para la venta en tu país, sino sólo para la venta desde una cuenta en Francia.
Si la redirección no se produce automáticamente, haz clic en este enlace.
Conectarme
Mi cuenta