Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.
Elimu ya juu aliipata chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.
Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni.
Kwa mujibu wa taarifa za intelijensia ndani ya Afrika nzima. Kuna mpango hatari sana uliyoundwa, ambao ungekuja kuhatarisha maisha ya bara zima. Hivyo kuzuia usitokee ndiyo suluhu tosha. Kitu ambacho watu wa usalama ndani ya umoja wa Afrika (AU) walikata shauri kukitimiza.
Majasusi watatu toka nchi tofauti wanateuliwa na kila mmoja kupewa jina bandia. Wanakutanishwa na kufanya operesheni hiyo ya siri kwa pamoja. Dhumuni kuu walinde bara zima, suala ambalo linawafanya wakutane na mapya. Yaliyowaacha mdomo wazi kwa kuona bara zima lilielekea kushikiliwa na wachache.
Kazi yao inayowachukua miezi haikuenda bure, walifanikiwa kunusuru hatari iliyoelekea kulikumba bara zima kwa ujasiri mkubwa.
Título : B. A. B. U
EAN : 9798230309642
Editorial : Mambosasa
El libro electrónico B. A. B. U está en formato ePub
¿Quieres leer en un eReader de otra marca? Sigue nuestra guía.
Puede que no esté disponible para la venta en tu país, sino sólo para la venta desde una cuenta en Francia.
Si la redirección no se produce automáticamente, haz clic en este enlace.
Conectarme
Mi cuenta