Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.
Elimu ya juu aliipata chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.
Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni.
Jasusi wa shirika la intelijensia na ulinzi Afrika ya mashariki (EASA) tawi la Rwanda, anatoweka kwenye mazingira ya kutatanisha, akiwa yu kazini akichunguza suala kutoweka kwa binti wa Bilionea.
Binti alipokuja kupatikana jasusi naye hakuonekana na wala kutambulika alipo. EASA hawakutaka kulifumbia macho suala hilo. Ilikuwa lazima mtu wao apatikane na sababu ya kutoweka kwake ijulikane. Maana hakuna kuku anayeweza kusahau kwao, kama hajarudi bandani basi amekutwa na jambo linalohitaji msaada wa ziada.
Ndipo hapo alipoteuliwa Norbert Kaila aliyekuwa mapumzikoni nchini humo. Baada ya kumaliza misheni yake aliyokuwa akiifanya Tanzania, akaishia kupewa likizo. Ila napo alikuja kusitishiwa na kutakiwa kurudi kazini, amtafute mwenzake alipo.
Mapya yanakuja kuibuka kwenye kazi hiyo, anapokutana na mtu ambaye alimdhani ndiye kumbe siye
Título : Sura Mbili
EAN : 9798230410935
Editorial : Mambosasa
El libro electrónico Sura Mbili está en formato ePub
¿Quieres leer en un eReader de otra marca? Sigue nuestra guía.
Puede que no esté disponible para la venta en tu país, sino sólo para la venta desde una cuenta en Francia.
Si la redirección no se produce automáticamente, haz clic en este enlace.
Conectarme
Mi cuenta