Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.
Elimu ya juu aliipata chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.
Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni.
Wanafunzi wa chuo wakiwa ndani ya mbuga ya wanyama ya Mkomazi, iliyochukua eneo la mkoa wa Tanga na Kilimanjaro nchini Tanzania. Walitega kamera zao kwa dhumuni la kunasa matukio ya maisha ya wanyama, ikiwa ni kazi waliyoifanya kwa ushirikiano mkubwa.
Matokeo ni kamera zile hazikunasa matukio ya wanyama, bali ni jambo ambalo halikutakiwa kuonekana na yeyote. Si kudhihirika tu, bali hata kusikiwa tu na ambaye hahusiki nalo haikufaa. Wenyewe hawakujua hilo hadi mambo yalipoanza kwenda mrama. Wanafunzi wale waliuawa na alibaki mmoja tu.
Huyo aliponea kwenye tundu la sindano asije kumalizwa, baada ya kuokolewa na mtu ambaye baadaye alikuja kufahamu alihitaji sana. mwishowe ndiyo ikaja kubainika alibeba ushahidi wa tukio la mauaji ya mtu muhimu sana kwenye serikali lililonaswa na kamera zile.
Título : Shuhuda
EAN : 9798230977629
Editorial : Mambosasa
El libro electrónico Shuhuda está en formato ePub
¿Quieres leer en un eReader de otra marca? Sigue nuestra guía.
Puede que no esté disponible para la venta en tu país, sino sólo para la venta desde una cuenta en Francia.
Si la redirección no se produce automáticamente, haz clic en este enlace.
Conectarme
Mi cuenta