Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.
Elimu ya juu aliipata chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.
Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni.
Asubuhi ya mapema, ambayo maafisa wawili wa polisi waliianza wakielekea ofisi. Hawakutaraji kama siku hiyo wangekuja kusikia jambo jingine jipya, wasilolitegemea kujiri kwenye mambo yo. Ndiyo hivyo hakuna ajuaye ya saa ya sekunde moja mbele.
Njiani wakakutana na kundi kubwa la watu. Walipolisogelea walibaini kuna mtu aliuawa na kutupwa. Mtu ambaye hakuwa mgeni sana machoni mwao, waliyozoea kumwona mara kadhaa na kushirikiana naye. ndiyo wakaja kuvaana na habari mbaya ya kifo chake.
Uchunguzi walipouanza tu na kufikia pazuri, maadui waliamua kuchukua hatua matokeo ni Afisa mmojawapo kujeruhiwa vibaya. Mwishowe kesi ikaja kuhamishwa kwenye mwanausalama mwingine, aliyeombwa msaada kutatua kitendawili hicho.
Makubwa yakaja kuibuka
Título : Kasiba
EAN : 9798230910046
Editorial : Mambosasa
El libro electrónico Kasiba está en formato ePub
¿Quieres leer en un eReader de otra marca? Sigue nuestra guía.
Puede que no esté disponible para la venta en tu país, sino sólo para la venta desde una cuenta en Francia.
Si la redirección no se produce automáticamente, haz clic en este enlace.
Conectarme
Mi cuenta