Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.
Elimu ya juu aliipata chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.
Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni.
Msafara wa kuhamisha pesa kutoka benki moja kwenda benki nyingine, ambao ulikuwa umepangwa kufanyika kwa usiri sana. Mpaka habari na mipango yake ikaandaliwa kikao cha siri sana, kilichohusisha wale tu ambao wangetakiwa kusafirisha na wakuu wao.
Janga linatokea baada ya njia ile iliyotakiwa kuwa wazi wakati msafara ukipita, kunakuwepo kwa foleni ambayo hawakuitaraji. Waliposimama ghafla, wanakumbana na majambazi ambao walionekana wazi kuwasubiri. Haikujulikana walijua vipi na matokeo hela zote zinaporwa na maaskari wa msafara kuuawa.
Kutokana na kuhisiwa kuna usaliti kati ya polisi waliyohusika kuandaa msafara ule, na hata benki ndiyo hapo inaamriwa upelelezi huo ufanywe n watu ambao hawatoki polisi. Matokeo ikaja kuangukia mikononi mwa EASA akapewa Norbert Kaila. Mazito yakaja kuibuliwa!
Título : Pesa Zangu
EAN : 9798227287069
Editorial : Mambosasa
El libro electrónico Pesa Zangu está en formato ePub
¿Quieres leer en un eReader de otra marca? Sigue nuestra guía.
Puede que no esté disponible para la venta en tu país, sino sólo para la venta desde una cuenta en Francia.
Si la redirección no se produce automáticamente, haz clic en este enlace.
Conectarme
Mi cuenta