Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.
Elimu ya juu aliipata chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.
Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni.
Biashara haramu ya uvunaji wa viungo vya binadamu na kuviuza, inashamiri nchini Tanzania. Ikifanyika kwenye hospitali na wengine ni wataalamu wa afya wakishiriki zoezi zima kwa manufaa ya wachache. Watu walifikia kuvuna viungo hivyo pasipo kuwashirikisha ndugu, au mtu mwenyewe kuacha usia afanyiwe hivyo mapema kabla hajafa.
Suala hilo linashindwa kufumbiwa macho na EASA, wanaamua kumwita Norbert Kaila mwenye utambulisho N001 kijasusi. Wanampatia jukumu la kuchunguza mtandao mzima na arejee na majibu. Kuanzia wahusika wote ni kina nani na pia wachukuliwe hatua.
Inambidi Kaila kuingia kazini kuchunguza ndiyo huko alipokuja kubaini biashara ile ilishikiliwa na wazito. Pia kuna sakata jingine la kitambo lililotokana na wazito hao, waliyojua limeisha kumbe walitafutiwa nafasi ya kufanyiwa kisasi kwa waliyoyafanya miaka hiyo.
Título : Operesheni Nyeusi
EAN : 9798227746658
Editorial : Mambosasa
El libro electrónico Operesheni Nyeusi está en formato ePub
¿Quieres leer en un eReader de otra marca? Sigue nuestra guía.
Puede que no esté disponible para la venta en tu país, sino sólo para la venta desde una cuenta en Francia.
Si la redirección no se produce automáticamente, haz clic en este enlace.
Conectarme
Mi cuenta