Hassan Mambosasa ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania, elimu yake ameipata kwenye shule mbalimbali za sekondari. Ikiwemo Jitegemee JKT, Wailes, Ubungo islamic, victory na kuja kuhitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Tambaza.
Elimu ya juu aliipata chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA), amesomea masuala ya TEHAMA akishughulika zaidi kwenye vifaa vya kompyuta.
Alianza uandishi mnamo mwaka 2006 hadi hii leo ameandika hadithi zaidi ya 40 katika mfumo wa vitabu vya mtandaoni.
Baada ya kuondolewa kwenye kesi aliyoisimamia kwa moyo mmoja. Ikiwa imebaki hatua ya mwisho kuelekea ushindi. Aliishia kulazimishwa apokee hundi ya milioni kumi. Ila aligoma na kuishia kuacha kazi moja, akiapa angeendelea na upelelezi kwa kutumia ujuzi wa sheria.
Asijue wabaya wale hawakupanga hilo litokee. Ndiyo hapo baada ya kunywa pombe kupunguza mawazo, akaja kuzima na kuamka akiwa kitandani. Kibaya zaidi pembeni yake kuwa binti mdogo umri chini ya miaka kumi na saba. Akitafakari hilo mlango unafunguliwa kwa nguvu wanaingia watu kadhaa wakiwemo polisi.
Inakuja kubainika binti alifariki dunia akiwa hapo kitandani, pia aliingiliwa kimwili na kifo chake kinasemekana kimetokana na dawa za usingizi zilizochanganywa na pombe. Kibaya zaidi ushahidi unamlenga yeye mwenyewe, na kuishia ndani.
Waliyoona nia wanajitokeza kumtetea, akiwemo Norbert Kaila na Wakili anayeitwa Grace. Mwishowe inakuja kubainika makubwa yaliyojificha nyuma ya sakata hilo.
Título : Jumba Bovu
EAN : 9798227318053
Editorial : Mambosasa
El libro electrónico Jumba Bovu está en formato ePub
¿Quieres leer en un eReader de otra marca? Sigue nuestra guía.
Puede que no esté disponible para la venta en tu país, sino sólo para la venta desde una cuenta en Francia.
Si la redirección no se produce automáticamente, haz clic en este enlace.
Conectarme
Mi cuenta